Taa maalum za kuwezesha kutua ndege usiku zimefungwa katika uwanja wa Ndege wa Songea mkoani Ruvuma hali ambayo utawezesha sasa ndege kutua usiku na mchana.
Hayo yamesemwa leo na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Ephatar Mlavi wakati anatoa taarifa ya upanuzi na uboreshaji uwanja wa Ndege Songea kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ambapo serikali imetoa shilingi bilioni 37 kutekeleza mradi huo.
Mhandisi Mlavi amesema mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya CHICCO ya nchini China umefikia asilimia 97 na kwamba mradi unatarajiwa kukabidhiwa Januari 30 mwaka huu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.