• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

NGOs zaaswa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya Taifa

Imewekwa kuanzia tarehe: June 29th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameyatahadharisha mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs)  kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya Taifa na kujiepusha na harakati zozote zinazokinzana na mila na desturi za kitanzania.

Kanali Thomas ametoa tahadhari hiyo wakati anafungua mkutano wa mwaka  wa mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani Ruvuma uliofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.

“Jiepusheni na kuchochea mahusiano ya jinsia moja,mkifanya hivyo serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa shirika lolote  lisilo la kiserikali litakaloshindwa  kufanya kazi kwa mujibu wa sheria,kanuni na miongozo’’,alisema Kanali Thomas.

Amesisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa na serikali bila kujali mchango unaotolewa na shirika hilo katika kuchangia maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma.

Hata hivyo Mkuu wa Mkoa ameyataja mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kuwa yanachangia maendeleo makubwa ndani ya Mkoa na Taifa kwa ujumla na kwamba serikali inatambua mchango huo ndiyo maana imeweka sera na sheria ili kuhakikisha NGOs  zinafanya kazi  kwa kuzingatia sera,sheria na miongozo.

Ameyaonya baadhi ya mashirika ambayo yanafanya kazi  bila kuzingatia miongozo ambapo amesema  yanajiweka katika hatari ya kufutwa katika orodha ya NGOs nchini.

Awali Mratibu na Msajili  wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoani Ruvuma Xsaveria Mlimira akitoa taarifa ya NGOs katika Mkoa amesema hadi sasa Mkoa wa Ruvuma una jumla ya NGSs 166 baada ya uhakiki ambao ulifanyika mwaka 2022.

Hata hivyo amesema katika Mkoa wa Ruvuma kuna mashirika nane kutoka nje ya nchi  ambayo yanashiriki katika shughuli za maendeleo kwenye sekta za afya,elimu na kilimo.

Ameyataja baadhi ya mafanikio ya NGOs mkoani Ruvuma kuwa ni kutoa mafunzo kwa watumishi katika vituo vya kutolea huduma za afya,kusaidia gharama za kufanya usimamizi shirikishi katika eneo la ukoma na kifua kikuu na kuchochea mahudhurio ya akinamama kujifungua yameongezeka kutoka asilimia 94 hadi 99 mwaka 2022.  

Mafanikio ya NGOs katika sekta ya kilimo ameyataja kuwa ni kukua kwa mitaji ya wakulima wadogo 10,000 toka shilingi milioni 80 mwaka 2019/2020 hadi kufikia shilingi bilioni 6.3 mwaka 2022/2023.

Katika mkutano huo mada mbalimbali zilitolewa zikiwemo sheria za mikataba,uandikishaji na uendeshaji wa mashirika  yasiyo ya kiserikali na kampeni ya  Mama Samia ya kutoa msaada wa kisheria kwa jamii ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Julai 22,2023 mkoani Ruvuma.

Mwisho

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.