MRADI wa Kiwanda cha vijana Chipukizi umezinduliwa pamoja na Mradi wa Redio Hekima FM 102.7 na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Lt.Josephine Mwambashi.
Akitoa Taarifa ya kikundi cha Vijana Mwenyekiti wa Kikundi cha Chipukizi Keneth Mbena amesema kikundi cha vijana Kata ya Kigonsera kilisajiliwa mwaka 2019 kikiwa na idadi ya wanachama 6 wenye umri kuanzia miaka 18 hadi 35.
Akielezea lengo la kuanzisha mradi huo ni kuongeza wigo wa ajira ambapo jumla ya wanufaika 15 wamejipatia ajira na kujiongezea kipato kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Hata hivyo Mbena amesema kikundi hicho cha vijana chipukizi kimefanikiwa kupata mkopo kutoka mfuko wa marejesho wenye zaidi ya shilingi milioni 22 na kununua mashine ya kuchanganya Saruji.
“Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru hadi kufikia Agosti 5,2021 wanakikindi tumefanikiwa kufyatua tofali 30,000 kwaajili ya ujenzi wa Jengo la ofisi ya Halmashauri na kupatiwa malipo ya shilingi milioni 9”.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa amekipongeza kwa kuamua kuunda kikundi na kufanya ujasiliamali na kuepuka kujiunga na makundi ya mtaani na kujiingiza katika madawa ya kulevya,na kuwapatia vijana wengine ajira.
Mwambashi ametoa rai kwa vijana kuendelea kuchangamkia fursa na kuacha kuwa tegemezi zaidi wawe wabunifu ili kuweza kujikwamua kiuchumi katika familia na kurejesha mkopo kwa wakati ili wengine nao wapate kupata mkopo huo.
Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo la Mbinga John Ndimbo amesema mradi huo umejengwa kwa kushirikiana na waumini wa Jimbo la Mbinga na ufadhili toka Jimbo ndugu(Wiirzburg) na kugharimu zaidi ya milioni 160.
Ndimbo amesema mradi huo ulianza kujengwa mwaka 2018 na kukamilika mwaka 2019 na kuanza kufanya kazi Oktoba 4,2019,na inasikika katika maeneo ya Wilaya ya Mbinga,Nyasa pamoja na maeneo ya Wilaya ya Songea.
Askofu Mkuu ameelezea Malengo ya kuanzishwa kwa redio hii ni pamoja na kutengeneza jamii yenye hofu ya Mungu ili iwezekuishi kwa amani na mshikamano,kukuza maadili katika makundi mbalimbali pamoja na kuhamasisha jamii kujikwamua kiuchumi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Habari Mkoa wa Ruvuma
Septemba 4,2021.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.