RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan (Chifu Hangaya) Septemba 23/2024 amefunga tamasha la tatu la utamaduni la kitaifa lililowaleta pamoja Maelfu ya watu kutoka ndani na Nje ya Tanzania.
Pamoja na Mambo mengine hotuba ya Mhe.Rais imetoa pongezi kwa wizara ya utamaduni,Sanaa na michezo kupitia kwa Waziri Mhe.Dkt.Damas Ndumbaro kwa kufanikisha kuratibu kwa umahiri tamasha hili ikiwa ni maagizo ya Mhe.Samia aliyoyatoa baada ya kufanyika kwa tamasha la kitamaduni la Bulabo huko Kanda ya ziwa Jijini Mwanza Miaka kadhaa iliyopita.
Rais Samia amewataka wananchi Mkoani Ruvuma na Taifa kwa ujumla kulitumia tamasha la utamaduni kama sehemu yakuimarisha umoja, upendo, mshikamano na utulivu ili kudumisha Mila, desturi na tamaduni za Kitanzania kwa kuwa ni kielelezo Cha uhai wa tamaduni hizi zilizorithiwa kutoka kwa Mabibi na Mababu.
Aidha Mhe Rais amewakumbusha watanzania kuufanya utamaduni kuwa biashara ili uwaletee faida za Kiuchumi,akitolea mfano ufundishaji wa kiswahili
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.