Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza muda wa msamaha wa kulipa kodi ya pango la ardhi bila riba kwa miezi mitatu hadi Aprili 30, mwaka huu.
Aidha, amewataka wananchi ambao wanadaiwa kodi hiyo, kulipa kabla ya muda wa msamaha uliotolewa kwisha.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Meandeleo ya Makazi, Dk. Angelina Mabula, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya wizara hiyo.
“Natoa rai kwa taasisi na mashirika ya umma na wananchi wote kutumia muda uliotolewa hadi Aprili 30 na Rais Samia kunufaika na msamaha wa riba uliotolewa kulipa deni la msingi ili wasamehewe riba ya malimbikizo ya kodi ya pango la ardhi,” amesema
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.