• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RAIS SAMIA atoa bilioni 145.77 kutekeleza mradi mkubwa wa maji Songea,mkataba wasainiwa

Imewekwa kuanzia tarehe: March 10th, 2023

SERIKALI inatarajia kuanza kutekeleza ujenzi wa mradi  wa maji wa miji 28 katika mji wa Songea mkoani Ruvuma unaogharimu shilingi bilioni 145.7.

Hayo yamesemwa Machi 10,2023 na Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso ambaye amewakilishwa na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Marypriska Mahundi  katika hafla ya utiaji Saini mkataba wa ujenzi wa mradi huo kati ya serikali  na Mkandarasi,  Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation.

“Mkataba  wa ujenzi wa mradi huo ni wa miezi 32 kuanzia Machi 10,2023,kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 katika mji wa Songea kutaleta manufaa makubwa ikiwemo SOUWASA kuongeza uwezo wa kuzalisha maji kutoka lita milioni 11.58 kwa siku hadi kufikia lita milioni 42.581 kwa siku,alisema Mheshimiwa Aweso.

Amesema mradi huo unakwenda kumaliza kero ya maji katika Manispaa ya Songea kwa sababu upatikanaji wa maji utakuwa uhakika na kwamba mradi una uwezo wa kuwahudumia wananchi wapatao 440,794.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba akizungumza kabla ya kusainiwa mkataba huo amesema  mradi huo utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia wananchi wa Songea hadi mwaka 2045, ambapo idadi ya wakazi  manispaa ya Songea inatarajiwa kuwa zaidi ya 400,000.

Amezitaja kazi ambazo zinatafanyika kwenye mradi huo ni ujenzi wa bwawa lenye uwezo wa kujaza maji lita milioni 4.8,ujenzi wa mtambo wa kuchuja maji lita milioni 16 kwa siku,ujenzi wa matanki ya maji  lita milioni tisa,kulaza mabomba yenye urefu wa kilometa 10.5 yatakayosafirisha maji kutoka kwenye mabwawa hadi kwenye matanki.

Katibu Mkuu  huyo wa Wizara maji. Amesema katika utekelezaji wa mradi huo kutakuwa usambazaji  wa maji wenye urefu wa kilometa zaidi  laki nane.

“Serikali imeamua kutekeleza mradi  wa maji miji 28 kwa kuangalia maeneo ambayo huduma ya maji haijawafikia wananchi ipasavyo,usanifu wa mradi huu unafanyika kwa miezi sita’’,alisisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) Mhandisi Patrick Kibasa amesema hivi sasa SOUWASA ina jumla ya vyanzo vya maji 13 vyenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 11.58 kwa siku ikiwa ni sawa na uzalishaji wa asilimia 57  ambapo mahitaji halisi ya maji kwa wananchi wapatao 286,285 kulingana na sensa ya watu ya mwaka 2022 ni lita milioni 20.336 kwa siku.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kuwa wananchi wa Ruvuma wanakuwa sehemu ya  kupata huduma ya maji safi na salama.

Kanali Thomas amesema Mkoa wa Ruvuma umepiga hatua kubwa katika utoaji huduma ya maji safi na salama ambapo hadi sasa utoaji huduma ya maji mijini umefikia asilimia 80.95  ambapo katika Halmashuri ya Manispaa ya Songea umefikia zaidi ya asilimia 90 na utoaji wa maji mjini Songea ni saa 22 kwa siku.

Hata hivyo amesema upatikanaji wa maji vijijini mkoani Ruvuma,kati ya vijiji  525 vilivyopo mkoani Ruvuma.vijiji 355  vinapata maji safi na salama sawana asilimia 67.

Naye Mbunge wa Songea mjini ambaye pia ni Waziri wa Sheria na Katiba Dkt.Damas Ndumbaro ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha hizo zinazotokana na mapato ya ndani ili kutekeleza mradi huo mkubwa wa maji.

Dkt.Ndumbaro amesema kutekelezwa kwa mradi huo  kunakwenda kumaliza kero ya maji katika mitaa yote 95 na kata zote 21 zilizopo Manispaa ya Songea ambapo amemuomba Mkandarasi wa mradi huo kumaliza kazi ndani ya mkataba.

SOUWASA ni miongoni mwa Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanzania Bara iliyoanzishwa mwaka 1997.

Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Machi 10,2023

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.