Rais Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 25 kutekeleza miradi ya maji katika wilaya ya Nyasa, ambayo inasimamiwa na RUWASA. Miradi hii inahusisha vijiji 34 vya wilaya hiyo na inatarajiwa kuboresha upatikanaji wa maji kwa wananchi zaidi ya laki mbili na elfu 120.
Mkuu wa wilaya ya Nyasa, Mhe. Peres Magiri, amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Rais Samia, miradi takribani 10 imekuwa ikitekelezwa, ikiwa ni pamoja na mradi wa maji wa Riyuli, ambao umegharimu bilioni 4.8 na kumalizika kwa mafanikio. Aidha, mradi wa Litui Group umepewa fedha za bilioni 6.5 na unatekelezwa, ambapo kata za Linga na Litui zitafaidika pindi utakapokamilika.
Diwani wa Kata ya Ngumbo, Mhe. Cosmas Nyoni, ameishukuru serikali kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji, ambayo inatarajiwa kutoa huduma kwa vijiji vitano, ikiwemo vijiji vya Ngumbo, Mbuli, Mkili, Yola, na Liyundi.
Mkazi wa kijiji cha Ngumbo, Mariana Mbonji, amepongeza juhudi za Rais Samia, akisema kuwa sasa wananchi wanapata maji karibu na makazi yao, jambo ambalo limewasaidia kuepuka adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.