• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RAIS SAMIA atoa bilioni 7.2 kujenga shule mpya za msingi 12 Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: March 5th, 2024

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 7.2 kupitia mradi wa BOOST kujenga shule 12 mpya za msingi  na miundombinu mbalimbali katika shule 44 mkoani Ruvuma.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema fedha hizo zimetolewa katika mwaka wa fedha za 2022/2023 na kwamba kati ya fedha hizo  zaidi ya shilingi bilioni 4.34 zimetumika kujenga shule mpya.

Amebainisha kuwa ujenzi wa shule hizo mpya umehusisha ujenzi wa madarasa ya msingi 98,madarasa ya elimu ya awali ya mfano 24,matundu ya vyoo ya elimu ya msingi 136 na matundu ya vyoo ya elimu ya awali 72.

Miundombinu mingine katika shule hizo ameitaja kuwa ni matundu ya vyoo vya walimu 24,vichomea taka 12 na majengo ya utawala 12.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa zaidi ya shilingi bilioni 2.9  zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ambayo inahusisha madarasa ya msingi 87,matundu ya vyoo ya msingi 114,madarasa ya  elimu ya awali 16,matundu ya vyoo vya awali 48 na nyumba za walimu mbili.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Ruvuma Mwl.Edith Mpinzile amesema Mkoa umepokea  shilingi milioni 264 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vya walimu 12 katika Halmashauri zote nane za Mkoa.

“Mkoa pia umepokea shilingi bilioni 1.56 kupitia mradi wa SWASH kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo 607 katika shule za msingi 47 na ujenzi upo katika hatua mbalimbali”,alisema Mpinzile.

Akizungumzia elimu maalum,elimu ya watu wazima na elimu nje ya mfumo rasmi,Afisa Elimu huyo Mkoa amesema hadi kufikia Novemba 2022,Mkoa ulikuwa na vituo 109 katika shule za msingi vinavyotekeleza mpango wa Elimu ya msingi kwa Watoto walioikosa (MEMKWA).

Amesema Mkoa wa Ruvuma hivi sasa una vituo 302 katika shule za msingi na sekondari vyenye Watoto wenye mahitaji maalum.

Hata hivyo amesema idadi ya Wanafunzi wasiojua KKK kwa darasa la kwanza na la pili imeendelea kupungua kutoka wanafunzi 7,427 mwezi Juni 2023 hadi kufikia 6,188 mwezi Desemba 2023 ikiwa ni sawa na asilimia 16.6.

Ameitaja mikakati ya kuinua elimu na kuongeza taaluma kuwa ni kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mtaala wa elimu katika ngazi za Halmashauri na shule,kuhimiza utoaji motisha kwa wanafunzi na walimu katika shule zinazofanya vizuri kwenye taaluma na kuhimiza wananchi utoaji chakula kwa wanafunzi wawapo shuleni.

Naye Mwalimu Mkuu shule mpya ya Msingi Nahange iliyojengwa kupitia mradi wa BOOST iliyopo Kata ya Suluti wilayani Namtumbo Mwl. Nahale Ponera amesema serikali imetoa shilingi milioni 331.6 kujenga shule hiyo  ambayo imeanza tangu

Amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 529 wanaosoma katika vyumba tisa  kuanzia awali hadi darasa la saba ambapo wanamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kutoa fedha za kujenga shule hiyo inayovutia wanafunzi kutokana kuwa na miundombinu ya kisasa.

Shaban Nyahale ni Mwanafunzi shule mpya ya msingi Mzalendo iliyopo Kata ya Masuguru wilayani Namtumbo amesema anamshukuru Rais Samia kwa kuwajengea shule yenye mazingira rafiki kwa kusomea.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.