• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RAIS SAMIA atoa vifaa tiba vya milioni 760 mkoani Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: March 6th, 2024

Na Albano Midelo,Songea

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 760  katika vituo 18 vya kutolea huduma za afya mkoani Ruvuma.

Hafla ya makabidhiano ya vifaa tiba hivyo kutoka Bohari Kuu ya Dawa (MSD) imefanyika kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma mjini Songea.

Akizungumza kwenye hafla hiyo mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema vifaa tiba hivyo vitasambazwa katika vituo 18 vya kutolea huduma za afya kwa  awamu mbili ambapo katika awamu ya kwanza itahusisha usambazaji wa vitanda vya hospitali,magodoro na mashuka.

Amesema vifaa hivyo vinasambazwa na MSD  Kanda ya Iringa na Mtwara kuanzia Machi 6,2024 kwenye vituo vilivyopo katika majimbo ya uchaguzi na Halmashauri za Mkoa wa Ruvuma.

“Ni Dhahiri kabisa ujio wa vifaa tiba hivi utasaidia kuboresha huduma za afya ,tunaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa katika sekta ya afya’’,alisema RC Thomas.

Kwa upande wake Mganga Mkuu  wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Louis Chomboko amesema vifaa tiba hivyo vimeletwa na serikali kwa mwamvuli wa majimbo tisa ya uchaguzi mkoani Ruvuma ili kuimarisha afya za wananchi hatimaye waweze kushiriki vema katika shughuli za maendeleo.

Hata hivyo amesema kutolewa kwa vifaa hivyo ni sehemu  tu ya  vifaa tiba kwa sababu serikali bado inaendelea kuleta dawa na vifaa tiba kupitia MSD ambapo katika kipindi cha kuanzia Julai 2023 hadi sasa Mkoa wa Ruvuma umepokea  shilingi bilioni 2.9 kutoka serikali kuu kwa ajili  ya ununuzi wa vifaa tiba.

Naye Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini Benaya Kapinga akizungumza kwa niaba ya wabunge wa Mkoa wa Ruvuma, amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta vifaa hivyo ambavyo amesema vimeleta faraja kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Komred John Haule amesema wataendelea kumpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwa anafanya vitu vinavyoonekana kwa wananchi.

Amewaasa watumishi wa afya mkoani Ruvuma kuhakikisha kuwa vifaa hivyo wanavitunza na vinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa

Ofisi ya Rais TAMISEMI imenunua vifaa tiba mbalimbali kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo katika majimbo 214 nchini yakiwemo majimbo tisa ya Mkoa wa Ruvuma

Kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Dr.Louis Chomboko akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas kuhusu vifaa tiba vilivyopokewa mkoani humo kwa ajili ya majimbo tisa ya uchaguzi ambavyo vitatumika kwenye vituo 18 vya kutolea huduma za afya

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.