Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan inaendelea kutoa mabilioni ya fedha kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wanapata huduma ya maji safi na salama.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amesema Mkoa unaendelea kutekeleza miradi ya maji 35 chini ya Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni 42.5.
Ameitaja miradi inayoendelea kutekelezwa kuwa ni Pamoja na miradi mikubwa ya Lituhi na Liuli iliyopo wilayani Nyasa ambayo inagharimu shilingi ya Bil.11.3 na itahudumia zaidi ya wakazi 52,285 waishio vijijini.
Amesema Mkoa wa Ruvumapia unatekeleza mradi mkubwa wa Maji katika Mji wa Songea kupitia programu ya Miji 28 kwa gharama ya shilingi bilioni 145.773
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.