Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza Ziara ya Kikazi Mkoa wa Ruvuma kuanzia Septemba 23 hadi 28 mwaka huu ambapo atafunga Tamasha la tatu la Utamaduni la kitaifa ambalo limefanyika kwa siku nne katika uwanja wa Majimaji Songea kisha Kuanza ziara ya kutembelea na kuzindua Miradi ya Maendeleo katika Wilaya zote za Mkoa Mkoa wa Ruvuma
Rais Samia akiwa mkoani Ruvuma pia atazungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed akizungumza na wanahabari ofisini kwake mjini Songea,amesema Rais akiwa mkoani Ruvuma atashiriki matukio matatu ambayo ni kufunga tamasha la utamaduni la tatu la kitaifa kwenye uwanja wa Majimaji mjini Songea siku ya Septemba 23,kuanza ziara ya kikazi katika wilaya zote kuanzia Septemba 24 hadi 27 .pia Rais Samia atashiriki Baraza la UWT Taifa litakalofanyika Manispaa ya Songea na kufunga kikao hicho Septemba 28.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.