RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi mkoani Ruvuma kuanzia Septemba 23 hadi 28 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed wakati anazungumza na wanahabari ofisini kwake mjini Songea.
Amebainisha kuwa akiwa mkoani Ruvuma Rais Samia Septemba 23 atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha Tamasha la Utamaduni la Kitaifa la tatu linalofanyika katika uwanja wa Majimaji..
Kulingana na Kanali Abbas ziara rasmi ya Rais Samia mkoani Ruvuma itaanza tarehe 24 hadi 28 Septemba 2024, ambapo atatembelea Wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma na kuzungumza na wananchi.
“Mheshimiwa Rais atafungua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kutumia fursa hiyo kuzungumza na wazee wa Mkoa wa Ruvuma’’,alisema.
Ameongeza kuwa Rais Samia atashiriki Baraza la Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UWT CCM) litakalofanyika katika Manispaa ya Songea na atafunga kikao hicho tarehe 28 Septemba 2024.
Amesema Rais atahitimisha ziara yake mkoani Ruvuma kwa kufanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Manispaa ya Songea katika uwanja wa Majimaji.
Ametoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote ambayo Rais atapita na kuzungumza na wananchi.
Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anafanya ziara ya kwanza ya kikazi mkoani Ruvuma tangu alipoingia madarakani kuwa Rais wa Awamu ya Sita.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.