RAIS wa Ujerumani Mheshimiwa Frenk-Walter Steinmeier amewasili nchini Oktoba 30 mwaka huu kwa ziara ya siku tatu.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Siku ya Novemba Mosi 2023, Mheshimiwa Rais Stenmeier atasafiri kuja Songea, mkoani Ruvuma kutembelea Makumbusho ya Taifa ya Majimaji na Shule ya Msingi ya Majimaji katika Manispaa ya Songea.
Makumbusho ya Taifa ya Majimaji ndiyo makumbusho pekee nchini Tanzania inayoonesha historia kubwa ya Vita ya Maji Maji katika harakati za ukombozi dhidi ya ukoloni wa Wajerumani.
Ndani ya Makumbusho hiyo kuna makaburi mawili ya mashujaa 67 walioonyongwa na wajerumani mwaka 1906.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.