Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Rehema Madenge akitabasamu ofisini kwake baada ya kukabidhiwa Tuzo zilizotolewa na Serikali baada ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kuwa miongoni mwa mikoa mitano nchini iliyoshinda Tuzo na Cheti kwa kuongoza kutoa habari kitaifa katika mwaka 2023/2024.
Washindi wa Tuzo hizo walitangazwa kwenye kongamano la wadau wa habari nchini lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kisha Tuzo hizo kukabidhiwa kwa washindi kwa niaba ya Rais na Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Nnauye
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.