Mkoa wa Ruvuma unashiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Wiki ya Uchangiaji wa Hiari wa Damu Salama, ambayo yameanza tarehe 1 Juni na yatakayofikia kilele chake tarehe 14 Juni 2025.
Maadhimisho haya ni sehemu ya kampeni ya kimataifa inayolenga kuhakikisha upatikanaji wa damu salama kwa watu wote wanaohitaji huduma hiyo muhimu ya kiafya.
Akizungumza wakati wa mkutano wa wadau uliofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea, Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amesema Serikali kupitia mkoa huo imejipanga kuimarisha huduma za afya kwa hatua mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya, ununuzi wa dawa, vifaa vya uchunguzi, pamoja na majokofu ya kuhifadhia na kusafirisha damu.
Kaulimbiu ya mwaka huu ya maadhimisho haya ni “Changia Damu, Leta Matumaini, Pamoja Tunaokoa Maisha”, ambayo inasisitiza umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari kama njia ya kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji.
Kwa mujibu wa takwimu zilizowasilishwa kutoka Januari hadi Mei 2025, Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kukusanya jumla ya chupa 2,952 za damu, ambayo ni sawa na asilimia 20 ya lengo la chupa 14,789 kwa mwaka huu.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.