Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa kutekeleza maagizo sita kati ya nane yaliyotolewa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) mwaka 2022.
Kanali Abbas ametoa pongezi hizo wakati anazungumza kwenye kikao cha kujadili utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya LAAC kilichofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea.
Hata hivyo amezitaja hoja za miaka ya nyuma katika Halmashauri hiyo ambazo bado hazijafanyiwa kazi kikamilifu ili ziweze kufungwa ni 12 na kwamba kuna hoja na mapendekezo 53 ambayo yanatakiwa kufungwa na kufanyiwa kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma pia ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kutekeleza maagizo Matano kati ya sita ya Kamati ya LAAC.
Katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea kati ya maagizo matatu yaliyotolewa na LAAC ni maagizo mawili yametekelezwa na kufungwa huku agizo moja utekelezaji wake haujakamilika kwa kipindi cha miaka minne sasa.
“Katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea jumla ya hoja na mapendekezo 44 bado hayajafanyiwa kazi ili yafungwe hivyo nawaomba waheshimiwa madiwani kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha hoja zote zinajibiwa ipasavyo’’,alisisitiza RC Abbas.
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika Halmashauri hizo,Mkuu wa Mkoa ameziagiza Halmashauri hizo kuhakikisha zinafanya maandalizi ya majibu ya hoja mapema na kwamba Halmashauri zichukue mapema hatua za kinidhamu kwa watumishi wanaozalisha hoja.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Mheshimiwa Menas Komba ameahidi kuhakikisha hoja zote zilizosalia katika Halmashauri hiyo zinajibiwa na kufungwa sanjari na kusimamia kasi ya ukusanyaji wa mapato.
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Michael Mbano,amesema Halmashauri imejitahidi kutekeleza maagizo sita ya LAAC na kwamba maagizo mawili yaliyosalia itayatekeleza ili yaweze kufungwa.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amefanya vikao vya kujadili utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya LAAC yaliyotolewa katika mwaka wa fedha wa 2021/2022 katika Halmashauri za Nyasa,Mbinga Mji, Namtumbo,Halmashauri ya Willaya ya Songea,Manispaa ya Songea na Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.