Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akiwakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Songea Pololet Mgema katika kumbukizi ya mashujaa wa Tanzania.
Akizungumza katika kumbukizi hizo zilizofanyika Manispaa ya Songea amesema Songea kuna Mashujaa waliopigana mwaka 1906 hadi 1907.
“ Tunao mashujaa mbalimbali Songea ni mfano mkubwa wa mashujaa walipigana mwaka 1906 hadi mwaka 1907 kutoka kabila la wangoni na Makabila mengine yaliyomo katika eneo hili ambalo lilikua likijulikana kama mji wa Ndonde”.
Mgema amewasihi wananchi kulinda uhuru haki na kuhakikisha katika Nchi kama ambavyo mashujaa wa vita waliamua kupoteza maisha yao ili kuilinda taifa letu.
Waziri wa Katiba na Sheria Damasi Ndumbaro amemshukuru Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suruhu Hassani kwa kuthamini siku ya mashujaa.
"Tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suruhu Hassani kwa kutenga na kukubali kuazimisha siku hii nchini kote ikiwa Kitaifa Maadhimisho yanafanyika Dodoma”.
Muhifadhi wa Makumbusho ya Taifa Songea Bathazali Nyamsiya katika Maadhimisho hayo amsema siku ya leo inajumuisha Mashujaa wote ikiwemo waliopigana vita Uganda waliolinda mipaka ya Nchi ya Tanzania na kutetea Maslahi mapana ya Taifa.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.