MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge ameongoza Sherehe za maadhimisho ya Miaka sitini ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Sherehe za Maadhimisho hayo imefanyika katika Viwanja vya Shule ya Muhuwesi Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma.
Ibuge amesema Miaka 60 iliyopita Tanzania Bara ilikata minyororo ya ukoloni Mwaka 1961 Mwasisi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwaongoza wananchi wa Tanganyika katika kuupokea uhuru.
’’Siku hiyo aibu ya takribani Miaka 77 ya kutawaliwa na wageni kutoka Ulaya ilifikia Ukomo tumetawaliwa na Waingereza Miaka 43 (1918-1961) na kabla yao miaka 34 (1884-1918) ya ukoloni wa Ujerumani’’.
Hata hivyo ibuge ameelezea mafanikio tangu kupata Uhuru Tanzania hadi kufikia sasa ikiwemo sekta ya Elimu hali ya Kielimu ilikuwa duni sana hivyo watu wengi walikuwa wanakabiliwa na ujinga.
Amesema Mwalimu Nyerere alitangaza ujinga kuwa moja ya maadui watatu ya nchi yetu pamoja na umaskini na maradhi,ilisababishwa na ufinyu wa kupata Elimu hasa kwa Waafrika ikisababishwa na Serikali ya Kikoloni.
’’Wakati tunapata Uhuru Mkoa ulikuwa na Shule za msingi 46 leo hii Mkoa una shule za msingi 818,shule za Sekondari zilikuwa 3 mpaka kufikia sasa Mkoa unashule za Sekondari 214, takwimu zinaonyesha mafanikio na kutufanya tutembee kifua mbele’’.
Akizungumzia upande wa Sekta ya Afya amesema mwaka 1961 Mkoa ulikuwa na Zahanati 8 na Hospitali 4 lakini mpaka kufikia sasa Mkoa wa Ruvuma una vituo 348 vinavyotoa huduma za Afya ikiwemo Zahanati 301 Vituo vya afya 34 na Hospitali 13.
Ibuge amezungumzia swala zima la Umeme kabla ya Uhuru mwaka 1961 hali ya upatikanaji wa Nishati ya Umeme ilikuwa Duni kwani isipokuwa baadhi ya maeneo machache,kwa sasa Mkoa umeunganishwa Umeme wa gridi ya Taifa katika Wilaya zote ikiwemo vijiji 319 vimepata na vijiji 235 vipo kwenye mpango.
Amesema sekta ya Miundombinu kabla ya Uhuru ulipopatikana Mkoa wa Ruvuma haukuwa na Mtandao wa Barabara za kiwango cha lami kwa sasa Barabara zina kiwango cha lami kilomita 700 za Barabara za kiwango cha lami ambapo Wilaya zote 5 zimeunganishwa katika kiwango cha lami.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Desemba 9,2021.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.