MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Brigdia Generali Wilbert Ibuge amefungua Mkutano wa jukwaa la Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori kusini mwa Tanzania zinazohusu fursa za uchumi.
Akizungumza katika ufunguzi wa Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Veta Manispaa ya Songea amsema Wataalamu Mkoa ,Wilaya na Mashirika yasiyo ya Kiserikali yapo kwaajili ya kuisaidia Serikali ya Mkoa wa Ruvuma kulinda na kuimarisha rasilimali kwa Manufaa ya Taifa.
“Utalii ni moja ya sekta zinazoongeza pesa nyingi za kigeni Nchini Tanzani,Utalii pekee huleta wageni takribani milioni 1.5 kwa mwaka,watali kuja Tanzania ili kufurahia wanyapori na kuchangia pato la Taifa asilimia 17 pamoja na kutoa ajira milioni 1.5”.
Hata hivyo Ibuge amesema ushoroba unakabiliwa na changamoto za uharibifu wa mazingira kama uchomaji wa moto,uvamizi wa maeneo ya hifadhi,ujagili na uvunaji haramu wa miti,pia Tanzania ilikuwa na robo ya Tembo wote barani Afrika na idadi kubwa ikiwa ni pori la akiba la Selous na idadi imepungua kufikia makadirio ya mwaka 2014 ni 15,000 hiyo inatokana na ujangili.
Kwa upand wake Mwnyekiti wa Muungano wa Jumuiya za Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania (CWMAC) Chrisopher Mademla ameishukuru Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuendelea kusaidia Muungano Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania katika kutekeleza Majukumu yake nchini.
“Nishukuru uongozi wa WWF Tanzania kwa kundela kufadhili miradi mbalimbali ya uhifadhi ukiwemo mradi huu wa kuongoza mabadiliko (SIDA Leading th Change) ambao ndio umeuwezesha kufanya mkutano huu muhimu”.
Mademla amewahakikishia kuwa Muungano utandelea kushirikiana kikamilifu na wadau wote wa uhifadhi wa Maliasili nchini hususani Serikali ili kuhakikisha rasilimali za nchi ya Tanzania zinalindwa kikamilifu kwa kuhakikisha kuwa tunapiga vita matumizi yote yasiyokuwa endelevu ikiwemo rasilimali za Wanyamapori.
Hata hivyo amesema kuwa Muungano unatambua na kuthamini mchango mkubwa wa jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuhimiza juu ya uhifadhi endelevu wa rasilimali za Wanyamapori katika Mkoa wa Ruvuma licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbalia mbazo zimekuwa zikikwamisha jitihada za uhifadhi wa Wanyamapori kutokana na wawekezaji.
Mademla ameelezea mafanikio ya Muungano huo kuwa kiunganishi muhimu katika Serikali na Jumuiya na kuyapatia ufumbuzi mambo mbalimbali yanayohusu uendeshaji wa WMAs nchini,imesaidia Jumuiya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kiuhifadhi kwa lengo la kuziwezesha kutekeleza majukumu.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Ruvuma
Septemba 13,2021
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.