Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameagiza kuundwa Tume mbili za kuchunguza matumizi ya fedha za mradi wa hospitali ya Wilaya ya Namtumbo ambayo hadi sasa serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni 2.8 kutekeleza mradi huo.
RC Thomas amemuagiza Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda kuchunguza matumizi ya fedha za ujenzi wa hospitali ya Namtumbo pia amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo Dkt Julius Ningu kuunda Tume ya kuchunguza matumizi ya fedha zilizotumika kwenye ujenzi wa hospitali hiyo.
kanali Thomas amezitaka Tume zitakazoundwa kutoa ripoti baada ya muda mfupi ili hatua zimeweze kuchukuliwa kwa yeyote atakayebainika kuhujumu mradi huo.
Mkuu wa Mkoa ameamua kuunda Tume mbili za Uchunguzi kufuatia ujenzi wa hospitali hiyo kusuasua na kutokamilika licha ya serikali kutoa fedha zote za kutekeleza mradi huo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.