Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kuboresha miundombinu ya zahanati ya kijiji cha Ruvuma kilichopo katika Kata ya Hanga hasa katika vyumba vya kujifungulia akinamama wajawazito ili waweze kupata huduma za uzazi kwenye mazingira bora na ya kuvutia.
Kanali Thomas ametoa maagizo hayo baada ya kukagua zahanati hiyo na kukuta akinamama wanapata huduma za uzazi kwenye mazingira yasiyoridhisha.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amefanya ziara ya siku moja katika wilaya ya Namtumbo ya kukagua miradi na kusikiliza kero za wananchi kwenye vijiji vya Mageuzi,Ruvuma na Mputa
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.