Mkuu wa Mkoa Kanali Laban Thomas amehaidi kurudi na kukagua miti yote iliyopandwa kwenye kila Shule amabayo imepewa miti ya kupanda kutoka kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
Hayo ameyasema wakati aliposhiriki kampeni ya upandaji miti katika Shule ya Sekondari ya Ruhuwiko iliyopo Wilaya ya Mbinga.
Kanali Thomas amewahimiza walimu na wanafunzi wasihishie kupanda miti hiyo na kuiacha bila kuifuatilia kwani Serikali imetumia fedha nyingi kuizalisha miti hiyo
“niwahakikishie nitapita mimi mwenyewe kukagua kila shule na kutazama miti yote ambayo wanafunzi wameipanda je! imestawi maana isiwe tunapanda miti pia na tuhakikishe inatunzwa na kustawi” amesema Kanali Thomas.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.