Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed amekerwa na kuchelewa kukamilika kwa miradi ya ujenzi wa Mahakama ya Wilaya na Chuo cha VETA Wilayani Tunduru ambapo ameagiza kasi iongezwe ili miradi hiyo ikamilike na kuanza kutumika.
Kanali Abbas ametoa maagizo hayo akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Tunduru ambapo amewaagiza wasimamizi wa miradi hiyo kuonesha mpango kazi unaotekelezeka ikiwemo upatikanaji wa rasilimali fedha za mradi kwa wakati,kuongeza nguvu kazi na kuhakikisha kazi inafanyika usiku na mchana.
“Kila jengo linajengwa kwa malengo ikiwemo kutoa huduma kwa wananchi hivyo iwapo majengo hayakamiliki maana yake watu hawahudumiwi,serikali imeamua kuwekeza na kujenga mahakama ya wilaya na Chuo cha VETA kuna mahali imeona huduma hizi zinasuasua’’,alisema.
Ameongeza kuwa serikali imeamua kuongeza majengo hayo kwa lengo la kuongeza huduma kwa wananchi hivyo amesema kuchelewa kukamilisha miradi hiyo ni kuirudisha nyuma serikali na mwisho wa siku lawama zinakwenda kwa Rais ambaye ameshamaliza kazi yake ya kutoa fedha za kutekeleza miradi hiyo ili ianze kutoa huduma.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hadi sasa imetenga shilingi bilioni 1.5 za kutekeleza mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Tunduru ambao unatarajia kukamilika Machi 2025.
Serikali pia imetoa Zaidi ya shilingi milioni 340 kuanza kutekeleza mradi wa chuo cha Ufundi Stadi VETA wilayani Tunduru kwa kujenga majengo tisa ambapo hadi sasa mradi umefikia Zaidi ya asilimia 60.
Mradi wa ujenzi wa mahakama ya Wilaya ya Tunduru ambapo serikali imetoa shilingi bilioni 1.5 kutekeleza mradi huo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.