Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, ameshuhudia makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Arusha kampasi ya Songea, ambapo bilioni 18 zitatumika kujenga chuo hicho katika kata ya Tanga mtaa wa Pambazuko.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika kata ya Tanga mtaa wa Pambazuko ambako chuo hicho kitajengwa, Kanali Ahmed amesema ujenzi wa chuo hicho si tu fursa kwa vijana kupata elimu ya juu, bali ni hatua madhubuti ya kupunguza gharama za masomo na kuondoa vikwazo vilivyowazuia wengi kutimiza ndoto zao.
Ameeleza kuwa ujenzi wa chuo hicho utatoa fursa nyingi za ajira kwa wakazi, huku ukichochea ukuaji wa uchumi kwa kuongeza thamani ya biashara, kuimarisha mzunguko wa fedha ndani ya mji, na kukuza sekta mbalimbali.
Naye Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Prof. Eliamani Sedoyeka, amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa bilioni 45 kwa chuo icho na kati ya hizo bilioni 18 zitatumika kujenga chuo hicho mkoani Ruvuma ambacho kutakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi zaidi ya 10,000.
Amebainisha kuwa fedha hizo zinaonyesha kuwa ni moja kati ya miradi mikubwa ndani ya mkoa wa Ruvuma, hivyo wanapaswa kusimamia ipasavyo ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, ameahidi ushirikiano wa karibu ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa mafanikio makubwa.
Hata hivyo Mbunge wa Songea Mjini ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, amekiri kuwa ni ndoto ya muda mrefu ya wananchi wa Songea na mkoa wa Ruvuma kuwa na Chuo kikuu ambayo hivi sasa inakwenda kutumia.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.