MKUU wa mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed ,amewataka wakazi wa mkoa huo hususani vijana kutumia mabonanza mbalimbali ya michezo kuhamasishana na kuelimishana juu ya umuhimu wa kwenda kujiandikisha kwenye Daftari la orodha la wapiga kura.
Amesema,kujiandikisha kwenye Daftari hilo kutawawezesha kuwa na sifa ya kupiga kura na kuchagua viongozi bora wanaowataka kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 27 Novemba mwaka huu.
Kanali Abbas amesema hayo ,wakati akifunga fainali ya mashindano ya Ruvuma vijana (vijana Ruvuma Cup 2024) kati ya Timu ya Bombambili City na Bombambili United iliyochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Sokoine Manispaa ya Songea.
Amesema,vijana wa mkoa wa Ruvuma wanapaswa kutumia mchezo huo kama hamasa ya kuendeleza michezo mingine hasa ikizingatiwa kuwa hivi sasa michezo imesaidia watu wengi kupata ajira.
Amempongeza mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi Kelvin Challe, kwa ubunifu wake mkubwa wa kuanzisha mashindano hayo yaliyowakutanisha vijana wengi kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Ruvuma.
Abbas,amewashukuru wadau waliosaidia kufanikisha mashindano ya vijana akiwemo Mbunge wa Vijana na Naibu Waziri wa Nishati Judith Kapinga aliyetoa jezi kwa timu zote zilizoshiriki Ligi hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Ruvuma Kelvin Challe,amewashukuru wananchi waliopata nafasi ya kushiriki Ligi hiyo kuanzia hatua ya awali hadi fainali.
Alisema,jambo la kujivunia mashindano ya mwaka huu yamekuwa yenye hamasa na mwitikio mkubwa kwani imeshirikisha jumla ya timu 32 ikilinganisha na msimu uliopita hasa baada ya kuongezeka kwa zawadi kwa washindi na timu zote shiriki.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.