JUMUIYA za watumia maji Bonde dogo la Mto Lutukila na Ruhuhu (JUWALURU) katika Halmashauri ya Madaba na Jumuiya ya watumia Maji Bonde dogo la Mtu Lumecha na Hanga (JUWALUHA) limezinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo ametoa rai kwa wanajumuisha kufanya kazi kwa kutenda haki na kuzingatia sheria zilizowekwa na kazuni zote.
“Sheria na kanuni zote mmezitunga wenyewe kwahiyo naomba mzingatie na kuwajibika”.
Mkuu wa Mkoa amesema wanajumuiya hizo kuhakikisha wanasimamia na kudhibiti shughuli mbalimbali ambazo zinachangia uharibifu wa vyanzo vya maji ikiwemo ulimaji wa vinyungu,ukataji miti,uchimbaji wa madini,ufugaji wa samaki na vingine vingi.
Akisoma taarifa kwa niaba ya Mkurugenzi wa Bonde la Ziwa Nyasa Samwel Yotham amesema mbali na kuandaa Jumuiya ya JUWALUHU na JUWALUHA Bodi ya maji ya Bonde la Ziwa Nyasa katika kutekeleza majukumu ya kuhifadhi,kutunza na kulinda Rasilimali za maji ili kujihakikisha upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Ruvuma.
Yotham amesema zimeundwa Jumuiya za Watumiaji Nne Bonde dogo la Mto Mbawa na Lwika (JUWABOHA),Jumuiya ya watumia maji mto Luwaita (JUWAMALU) na Mto Mungaka (JUWAMU) Wilaya ya Mbinga,Jumuiya ya Watumia Maji Mto Luhira na (JUWALU) Wilaya ya Songea.
Amesema vimejengwa vituo 14 vya kufuatilia mwenendo wa Maji (vituo 2 vya Halali ya Hewa eneo la Shule ya Msingi ya Madaba na Shule ya Msingi Mbambabay na eneo la Shule ya Msingi Paradiso Mbinga pamoja na Nyasa Ruhuhu Masigira kijiji cha Mahanje Madaba.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Septemba 26,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.