MKOA wa Ruvuma umeshika nafasi ya nne katika utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kupitia tathmini sita katika tathmini tatu za mwisho.
Hayo amesema Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas katika usainishaji wa Mkataba wa usimamiaji wa shuguli za Lishe.
“Mkoa ulishika nafasi ya nane Mwaka 2019/2020 nafasi ya pili Mwaka 2020/2021 na nafasi ya nne Mwaka 2021/2022”.
Amesema Mkoa unatakiwa kufanya Tathimini ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe mara mbili kwa Mwaka kila baada ya miezi sita na awamu ya mwisho ya Tathimini ilifanyika mwezi Agosti 2022 ikiwa Halmashauri zinatakiwa kufanya Tathmini kila robo Mwaka.
Thomas ametoa rai kwa watendaji wote kuwa Mkataba utasaidia kubaini changamoto zilizopo katika maeneo yote na kuchukua hatua mathubuti za kupunguza hali duni ya Lishe hususani udumavu wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
“Tutasimamia vizuri kwa weledi utekelezaji wa Mkataba huu ili tuweze kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania “.
Hata hivyo amesema Ofisi ya Rais TAISEMI kwa kushirikiana na Mkoa ilifanya uhakiki wa Taarifa za Lishe hususani matumizi ya fedha ripoti inaonyesha kutofautiana kwa taarifa zilizowasilishwa na Halmashauri.
“Niwaelekeze kuhakikisha fedha zilizopangwa kutekeleza shughuli za lishe zinatolewa kupitia vifungu sahihi na zitekelezwe shughuli pangwa”.
Amesema Mabalozi wa Lishe wateuliwe katika maeneo yote kuanzia ngazi ya Halmashauri hadi kata kwa lengo la kuongeza hamasa kwa wananchi wote kujua umuhimu wa Lishe pia Mkoa umemteua Mhe. Mhandisi Stella Manyanya Mbunge wa Nyasa kuwa balozi wa Lishe Mkoa akishirikiana na Jackline Msongozi.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Octoba 11,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.