Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas amewaapisha wajumbe wanne wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Namtumbo.
Wajumbe hao walioapishwa katika hafla iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Songea ni pamoja na Kisuu Mtimda,Longinus Mhagama,Fatuma Mapunda na Mecktilda Chiwango .
Wajumbe hao wataliongoza Baraza hilo kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Aprili 30,2024.
Akizungumza baada ya kuwaapisha wajumbe hao Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma amewapongeza kwa kupata nafasi hiyo ambapo amewataka kutenda haki bila upendeleo .
“Wilaya zina migogoro mingi ya ardhi,mabaraza ya ardhi kazi yake ni kufanya usaidizi ili kupunguza changamoto za migogoro ya ardhi katika wilaya “,alisisitiza.
Kanalı Abbas ameshauri kila Mjumbe kuhakikisha anatenda haki kulingana na kiapo chake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Songea Ismail Ayo amesema wajumbe hao wameapishwa kwa mujibu wa kanuni za Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya za mwaka 2003 .
Ayo amesema wananchi wa Namtumbo hivi sasa wataepuka aza kubwa kusafiri hadi Songea kufuata huduma ya Baraza la Ardhi na Nyumba
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.