Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameipongeza Idara ya Mahakama Kuu Kanda ya Songea kwa kupiga hatua kubwa katika utoaji haki hasa baada ya kuboresha miundombonu ya mahakama ikiwa ni Pamoja na matumizi ya TEHAMA.
Ametoa pongeza hizo wakati anazungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini ambazo kimkoa zimefanyika kwenye viwanja vya Mahakama Kuu,Kanda ya Songea.
RC Thomas ameipongeza Mahakama Kuu Kanda ya Songea kwa kutatua changamoto ya mlundikano wa mashauri ambapo hivi sasa mashauri yenye muda mrefu yamebakia machache.
Ameipongeza Mahakama hiyo kwa kupeleka vifaa vya TEHAMA katika magereza ya Tunduru na Mbinga ambavyo vinakwenda kutumika kwa ajili mfumo wa jumuishi wa haki jinai kwa ajili ya kusikiliza mashauri kwa njia ya mtandao.
Amesisitiza kuwa juhudi zinazofanywa na vyombo vyote vya haki jinai zina mchango mkubwa kwa jamii ambapo ameshauri kushirikiana ili kuunganisha mifumo ya utendaji kazi hatimaye kufikia mafanikio makubwa katika utoaji haki.
Kaulimbiu ya mwaka huu kwenye maadhimisho ya siku ya sheria nchini inasema umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa;nafasi ya mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi na haki jinai.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.