• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC RUVUMA awatahadharisha wakandarasi "Sitapokea miradi iliyojengwa chini ya kiwango''

Imewekwa kuanzia tarehe: November 1st, 2022

MKUU wa mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema,hayuko tayari kuona  wala kupokea  miradi ya barabara na miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa katika mkoa huo  iliyojengwa chini ya viwango.

Kanal Laban amesema hayo  leo, wakati wa hafla ya usainishaji mikataba 13 ya ujenzi wa miundombinu ya barabara,madaraja na makalavati kati ya Wakala wa barabara za mjini na vijijini(TARURA)mkoa wa Ruvuma na  wakandarasi yenye thamani ya Sh.bilioni 6,128,065,525.00 inayokwenda kutekelezwa katika mkoa huo.

Wakandarasi hao wakiongozwa na kampuni ya Ovans Contruction Ltd, wanakwenda kujenga barabara kwa kiwango cha lami, changarawe,madaraja na makalavati katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Ruvuma.

Kanali Laban alisema,fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo  zimeshatengwa, na kuwataka wakandarasi  kwenda kufanya kazi  walizopewa kwa wakati kabla ya mvua za masika hazijaanza kunyesha ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza.

“leo wakandarasi mmesaini mikataba mbele yangu,fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara  zipo,hakikisheni mnakwenda kujenga barabara za viwango na mnakamilisha  kazi kwa muda uliopangwa kama mikataba yenu inavyosema,TARURA sitaki kusikia mnaongeza muda wa ujenzi kwa mkandarasi”alisisitiza Kanal Laban.

Alisema,wananchi wa mkoa wa Ruvuma wanataka barabara zenye viwango zitakazodumu kwa miaka mingi na siyo ndani ya mwaka mmoja zinaanza kufanyiwa matengenezo

Mkuu wa mkoa,amewapongeza wakandarasi walioshinda zabuni hizo na kuwataka kwenda kutekeleza miradi hiyo kwa kuzingatia ubora na muda uliopangwa kwani zikiboreshwa zitachochea ukuaji uchumi wa wananchi na kuboresha  sekta ya kilimo ambayo ni uti wa mgongo wa wananchi wa mkoa huo.

Aidha amesisitiza kuwa, mkandarasi atakayejenga barabara na miradi mingine ya maendeleo chini ya kiwango atashughulikiwa na hatopata kazi yoyote katika mkoa wa Ruvuma.

“ninyi ni wakandarasi wazawa,nawaombeni sana kafanyeni kazi zenu kwa ufanisi mkubwa na mshindane na wakandarasi wa nje,Ruvuma tunahitaji barabara nzuri na zenye viwango zitakazo chochea kukua kwa uchumi wa wananchi na mkoa wetu”alisema.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho amesema,amefurahishwa  sana kuona wakandarasi wazawa wakiendelea kuaminika,kupata na kufanya kazi za ujenzi wa barabara na miradi mbalimbali.

Alisema,barabara zinazokwenda kujengwa katika maeneo mbalimbali zitakuwa chachu ya maendeleo na   kuwa kiungo muhimu cha ukuaji wa uchumi wa mkoa wa Ruvuma,na  Chama cha Mapinduzi kina imani kubwa na wakandarasi hao watatimiza wajibu wao.

Mwenyekiti huyo wa Chama cha Mapinduzi, amewaasa  wakandarasi walioshinda zabuni hizo kwenda kutekeleza miradi hiyo kwa ufanisi huku akiwataka TARURA  kuwa makini kusimamia ujenzi wa barabara hizo kwa hatua zote za utekelezaji wake.

Naye Meneja wa TARURA mkoa wa Ruvuma Mhandisi Wahabu Nyamzungu amesema,  Tarura imeingia mikataba 40 na Wakandarasi katika hatua ya kwanza yenye jumla ya Sh.bilioni 13,173,296,710.00 kwa ajili ya  kutekeleza kazi mbalimbali za matengenezo ya barabara,ujenzi wa madaraja na makalavati kwa mfuko wa  fedha wa barabara,jimbo na tozo.

Alisema,hadi kufikia mwezi Septemba 2022 miradi yote 40 inaendelea kutekelezwa na ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wake, na katika bajeti iliyotengwa   kwa ajili ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ni Sh.bilioni 6,128,065,525.00.

Alisema,mikataba iliyosainiwa katika awamu ya pili (Phase 11) kati ya TARURA na Wakandarasi  ni asilimia 40 na itahusisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha  lami changarawe,madaraja na makalavati katika mkoa wote wa Ruvuma.

Amefafanua kuwa, mikataba hiyo inahusisha mikataba mitano ya jimbo inayogharimu Sh.bilioni 2,481,325,500.00,mikataba sita ya tozo yenye thamani ya Sh.bilioni 2,639,562,475.00,mkataba mmoja wa matengenezo kupitia mfuko wa barabara utakaogharimu kiasi cha Sh. milioni 294,903,000.00.

Ameongeza kuwa,mkataba mmoja ni wa fedha maalum kutoka Serikali kuu utakaogharimu jumla ya Sh.milioni 712,274,500.00 ambao utekelezaji wake umeanza mwezi Oktoba  2022 na utamalizika mwezi Februari 2023.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.