• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

RC RUVUMA awataka wazazi na walezi kuchangia chakula cha mchana kwa watoto wao

Imewekwa kuanzia tarehe: May 21st, 2023

Mkuu wa mkoa,amesema hayo jana wakati akizungumza na wanafunzi,walimu na baadhi ya wazazi wakati wa ziara yake ya kuhamasisha zoezi la upandaji miti katika Manispaa ya Songea mkoani humo.

Amewataka wazazi na walezi kuwa na huruma na kuona umuhimu wa kuanza kuchangia chakula ili kuwawezesha watoto kuwa na usikivu darasani jambo litakalowasaidia kufanya vizuri katika masomo yao.

Alisema,ni jambo lisilovumilika  hata kidogo kuona mkoa wa Ruvuma unaongoza kwa kuzalisha chakula,lakini baadhi ya wazazi wanashindwa kuchangia chakula na hivyo kuwapa wakati mgumu walimu kutafuta chakula kwa ajili ya watoto hao.

Amewataka kubadilika kifkra na kuona aibu kwa kuwa hilo ni jukumu lao na siyo la serikali,hivyo ni lazima wawajibike kwa kuwapatia watoto  wao mahitaji muhimu ikiwemo chakula na mavazi.Aidha,Mkuu wa mkoa amepiga marufuku tabia ya wakulima kuuza mazao hasa mahindi yakiwa bado shambani,badala yake kusubiri hadi soko la uhakika litakapofunguliwa.

Alisema,ana taarifa kwamba wafanyabiashara wameanza kupita mashambani na kuwashawishi wakulima kuwauzia mahindi kwa bei ya Sh.1,000 hadi 1,200 kwa kilo moja ambayo hailingani na gharama ya uzalishaji mashambani.

Amewaonya wafanyabiashara kuacha mara moja tabia hiyo kwani serikali imejipanga kuchukua hatua kali kwa mtu na mfanyabiashara atayekamatwa anawarubuni wakulima ili wauziwe mahindi yakiwa bado shambani.

“ndugu zangu niwaambie mwaka huu mahindi yatakuwa na bei nzuri sana kwani baadhi ya mikoa ikiwemo Lindi,Mtwara,Pwani na Tanga hali ya uzalishaji wa chakula siyo nzuri kutokana na upungufu wa mvua”alisema.

Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa,kutokana na changamoto hiyo mahitaji ya chakula katika maeneo  hayo ni makubwa,na kuwasihi wakulima kuendelea kuvuta subira hadi soko la uhakika litakapofunguliwa.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Songea Wilman Ndile alisema,serikai ya wilaya imejipanga kuhakikisha hakuna mfanyabiashara anayekwenda  mashambani kushawishi wakulima ili auziwe mahindi na mazao mengine yakiwa bado shambani.

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MBINGA-MBAMBABAY : barabara inayojenga utalii kwenye milima ya Kusini

    June 01, 2025
  • PICHA ya Rais Samia yapamba mti wa kihistoria Namtumbo

    June 01, 2025
  • TAIFA lamlilia Songambele Shujaa wa Uhuru aliyeishi karne moja

    June 01, 2025
  • SHAMBA la AVIV Tanzania ni mfano wa kuigwa nchini

    June 01, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.