MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameogoza hafla fupi ya usainishaji wa mkataba wa usimamiaji wa shughuli za Lishe na Wakuu wa Wilaya za Mkoa.
Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Kamanda wa Brigedi Chandamali Manispaa ya Songea na kuhudhulia viongozi wa Taasisi mbalimbali za Mkoa.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa amesema suala hilo la usimamiaji wa Mkataba wa Lishe limekuwa likifanyika kwa miaka mitano kuanzia ngazi ya Wizara,Mkoa hadi Ngazi ya kijiji.
Amesema lengo ni kuhakikisha Mkoa na Halmashauri unasimamia ipasavyo utekelezaji wa afua za Lishe na kuchukua hatua mathubuti za kupunguza hali duni ya Lishe katika maeneo yote.
“Serikali inatambua kuwa bado zipo changamoto nyingi katika kukabiliana na utapiamlo hapa nchini ikiwa changamoto kubwa kuliko yote ya kuongeza uelewa wa masuala ya lishe”.
Hata hivyo amesema Serikali ilisainishana Mkataba wa usimamiaji wa Shughuli za Lishe kati ya Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa wa Tanzania Bara Octoba 3,2022 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mwaka wa tathimini ya sita ya utekelezaji wa Mkataba wa Lishe Jijini Dodoma.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Neema Magembe amesema kwa kushirikiana na Wakuu wa Wilaya watahakikisha wanatenga elfu moja kwa kila mtoto na kuhakikisha inafanya kazi katika suala zima la Lishe.
Magembe amesema pia katika viashiria vyote vilivyopo katika mkataba wa Lishe watahakikisha vinatekelezwa kwa usahihi ikiwa mkataba huo Mkuu wa Mkoa amewasinisha Wakuu wa Wilaya nao watawasainisha Wakurugenzi kwaajili ya utekelezaji.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde
Kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Octoba 11,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.