Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amewataka viongozi na watumishi wa serikali kutojihusisha kuchukuwa tenda za ujenzi wa miradi ya Serikali.
Hayo ameyasema wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya uboreshaji miundombinu ya shule za msingi na shule za awali (BOOST) katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na Wilaya ya Nyasa
Amesema kama kuna viongozi wanahusika kuchukua tenda katika ujenzi wa miradi hiyo waache mara moja kwani wao wanachangia kwa kiasi kikubwa kudhohofisha kasi ya utelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi
“Kwa wale viongozi wote aidha wakuchaguliwa au wakuteuliwa tuache kuingiza mikono yetu aidha kwa kuchukua tenda za kuleta vifaa vyovyote kwenye haya maeneo ya ujenzi sisi ndio tusimamie miradi hii tuache kupiga madili”
Hata hivyo amewataka wananchi kuacha tabia ya kutohoji na kuwatetea wataalamu na mafundi pale wanapoziona dosari katika miradi watoe taarifa kwani miradi hiyo inajengwa kwa faida ya watoto wao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.