Mkoa wa Ruvuma unaendelea kuwapanga wafugaji kwenye vitalu kwa mfumo wa ranchi ndogo na kudhibiti uingiaji holela wa mifugo.
Kwa Mujibu wa Afisa Mifugo Mkoani Ruvuma Nelson William ameeleza kuwa wafugaji 125 wenye ng'ombe 38000 kati ya wafugaji 145 walioingia kiholela Wilayani Tunduru wakiwa na ng'ombe 62000 wamepangwa kwenye vitalu 191 sawa na Asilimia 83 ya lengo la kuwapanga wafugaji mbalimbali wa Ng’ombe,Mbuzi ,Punda na Kondoo.
Hata hivyo amesema kumekuwepo na ongezeko la mifugo inayochungwa holela katika maeneo kadhaa ya Mkoa yakiwemo mashamba ya wakulima na Katika hifadhi za Taifa na misitu ya kijamii, na waliopangiwa kwenye vitalu kutoka kwenye maeneo hayo .
Amesema kuwa hali hiyo imejitokeza zaidi katika wilaya ya Namtumbo na Tunduru na Kusababisha kutoelewana baina ya wakulima na wafugaji.
Aidha,Mkoa ulibainisha njia kuu iliyotumiwa na wafugaji hao kuingia kinyemela katika Mkoa wa Ruvuma wamepitia kijiji cha Kitanda wilayani Namtumbo.
William alieleza kua Mkoa umeendelea kudhibiti uingiaji holela wa Mifugo kwa kuwabainisha wafanyabiashara wa Mifugo na wafugaji wanaoshiriki katika uingizaji wa mifugo kiholela
Amesema Wafanyabiashara 4 na wafugaji 13 wenye ng'ombe 1045 na mbuzi 38 kwa mwaka 2017/2018 na ng'ombe 94 mbuzi 15,kondoo 10 na punda 5 kwa kwa mwaka 2018/2019 na ng'ombe 1800 kwa mwaka 2019/2020 walikamatwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba.
“Tunduru na Songea Wamechukuliwa hatua kwa kutozwa faini jumla ya shilingi 9,200,000.00 kwa mwaka 2017/2018.Shilingi 700,000.00 kwa mwaka 2018/2019 na shiling 7,000,000.00 kwa mwaka 2019/2020”.
Hata hivyo amesema Pamoha na faini hizo walirudishwa na mifugo yao huko walikotoka ikiwa Mkoa umetenga hekta 281,217 kwa ajili ya kupokea mifugo inayoondolewa kwenye hifadhi ya misitu na maeneo ya kilimo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.