Mkoa umekuwa katika mstari wa mbele katika kuhamasisha jamii juu ya upandaji miti na utunzaji mazingira.
Uhamasishaji huu huenda sanjari na utekelezaji wa kampeni ya kitaifa ya upandaji miti ambao hufanyika kila mwaka kwenye Halmashauri zote.
Mkoa wa Ruvuma una lengo la kupanda miti kibiashara ekari 100,000 kwa muda wa miaka kumi (10) toka 2015 – 2025.
Mradi huu utatekelezwa katika maeneo ya Serikali, vyuo na shule,Kwa msimu wa mwaka 2023/24 Mkoa wa Ruvuma umepanda jumla ya miche ya miti 4,099,014 ambapo imepandwa katika Halmashauri zote, miti hii ni kwa ajili ya mbao, vyanzo vya maji na matunda.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.