Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Mheshimiwa Peres Magiri, amebainisha kuwa mwitikio wa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na maeneo mengine ya nchi bado ni mdogo katika kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo mkoani Ruvuma.
Amebainisha hayo wakati akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed katika hafla ya Toyota Networking Cocktail iliyofanyika katika ukumbi wa kanisa la Anglican mjini Songea, ikiwa ni maandalizi kuelekea tamasha la Toyota litakalofanyika Juni 2025.
"Pamoja na uwepo wa vivutio katika mkoa wetu, bado mwitikio wa kutembelea vivutio hivyo umekuwa ni mdogo sana hasa kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma, watanzania kwa ujumla na wageni kutoka nchi zingine kuja Ruvuma kutembelea vivutio hivyo,"alisema Mhe. Magiri.
Ameongeza kuwa Mkoa kwa kushirikiana na wadau wakiwemo Wategi Traders Company wamekusudia kufanya tamasha hilo likiwa na lengo la kuvitangaza vivutio vilivyopo ndani ya mkoa ili kuunufaisha mkoa kwa kuwezesha kuingiza fedha za kigeni na kukuza pato la Mkoa pamoja na kuwafanya wadau kuwa na utamaduni wa kutembea vivutio hivyo.
Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Bi. Mary Makondo amesema kwa ushirikiano wataweza kufanikisha kulifanya tamasha hilo kwa ukubwa hivyo kila mtu ana kitu cha kufanya ili kufanikisha tamasha hilo ambalo litajumuisha magari aina ya Toyota zaidi ya 5,000.
Kwa upande wake Kamanda wa TFS Kanda ya Kusini SACC Manyisye Mpokigwa amesema siku iliyopangwa kwa ajili ya tamasha la Toyota itasaidia vituo mbalimbali vilivyopo ndani ya mkoa kufahamika.
Hata hivyo Afisa Utalii wa Pori la Akiba la Liparamba, Maajabu Mbogo, amesema kama wadau wamejipanga kuvitangaza vivutio mbalimbali vya utalii kama vile hifadhi ya visiwa vya Lundo na Ruhila Zoo kupitia tamasha hilo.
Mkoa wa Ruvuma unajivunia kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Nyerere, Makumbusho ya vita ya Majimaji, Pori la akiba la Liparamba na fukwe za Ziwa Nyasa na vingine vingi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.