Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bi. Mary Makondo, amewaongoza watumishi wa umma na wananchi wa mkoa wa Ruvuma kufanya usafi wa mazingira maeneo mbalimbali katika kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania Bara .
Usafi huo umefanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Songea (HOMSO), Soko kuu la Songea na kuhitimisha katika kituo cha mabasi kilichopo Mfaranyaki Manispaa ya Songea.
Akihitimisha zoezi hilo, Makondo amewataka wananchi wa mkoa wa Ruvuma kujijengea utamaduni endelevu wa kufanya usafi kwa kuwa uchafu ni chanzo cha Magonjwa.
Amewasisitiza wananchi kutotupa taka hovyo katika maeneo yao ya kazi, biashara na majumbani ili kuhakikisha mji unakuwa safi kama miji mingine.
"Tufanye Manispaa ya Songea ipendeze tuwe kama miji mingine ambapo tumeona usafi ni kipaumbele, viongozi wa mitaa kuwasimamia wananchi kukusanya taka, tunataka tuone mji wetu ukipendeza zaidi, na hii tabia iwe ya kudumu," alisema Makondo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dr. Louis Chomboko, amesema usafi na magonjwa ni ndugu hivyo kwa kufanya usafi wananchi wataondoa magonjwa na kuimarisha mwili kutopata magonjwa.
Mkoa wa Ruvuma umeungana na mikoa yote nchini kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa kufanya usafi wa mazingira katika majengo ya umma na kuwahamasisha wananchi kudumisha usafi.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.