Katika uongozi wa serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Mkoa wa Ruvuma umeshuhudia mageuzi makubwa yasiyo na kifani katika sekta ya afya, kwa kutumia zaidi ya shilingi bilioni 45.3 kuboresha huduma kwa wananchi.
Kiasi hicho kikubwa cha fedha kimewezesha ujenzi wa hospitali tano za wilaya, vituo vya afya 16 na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – hatua inayomaanisha kuwa wananchi waliokuwa wakisafiri mamia ya kilomita kutafuta huduma, sasa wanazitumia karibu na makazi yao.
Mapinduzi haya ya afya yameenda sanjari na ujenzi wa majengo manne ya kisasa ya huduma za dharura (EMD), ujenzi wa zahanati 47 vijijini, pamoja na ununuzi wa magari 21 ya kubeba wagonjwa.
Serikali pia imenunua magari saba kwa ajili ya ufuatiliaji wa shughuli za afya, magari matano kwa usambazaji wa chanjo na gari moja mahususi la huduma za lishe—yote ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuhakikisha afya bora kwa kila mwananchi wa Ruvuma.
Mafanikio haya makubwa yanayoendelea kuvuta hisia za watanzania wengi, si tu yanapunguza vifo vinavyoweza kuzuilika bali pia yanadhihirisha dhamira thabiti ya serikali kuwekeza katika maisha ya watu. Mkoa wa Ruvuma sasa ni kielelezo cha mkoa unaoinuka kwa kasi, ukiwa na miundombinu bora ya afya, watumishi waliopata mafunzo, na huduma zinazokidhi mahitaji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.