WIZARA ya maji kupitia wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,imeanza kutekeleza miradi ya maji katika vijiji mbalimbali ambavyo kwa muda mrefu havikuwa na huduma hiyo.
Kaimu Meneja wa Ruwasa wilaya ya Namtumbo Salum Nachundu, alitaja miradi hiyo ni pamoja na mradi wa maji Mkongo Gulioni-Nahimba uliotekelezwa chini ya Programu ya maendeleo ya sekta ya maji(WSDP)kupitia program ndogo ya maji na usafi wa mazingira vijijini(RWSSP).
Alisema, mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2017na mkandarasi Kipera Contractors ambaye alitakiwa kukamilika kazi mwaka 2020,lakini alishindwa kukamilisha kazi kutokana na changamoto mbalimbali ikiwamo uwezo mdogo wa kiufundi na fedha.
Nachundu alieleza kuwa,baada ya Serikali kukatisha mkataba na mkandarasi, mradi huo umekamilishwa na wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa) kwa njia ya force akaunti ambapo kwa sasa umekamilika na wananchi wanapata huduma.
Kwa mujibu wa Nachundu,mradi wa Mkongo gulioni-Nahimba ulisanifiwa kuhudumia wakazi 8,007 katika vijiji hivyo ambapo awali gharama ya mradi ilikuwa Sh.2,069,975,521,hata hivyo zilipungua hadi Sh.1,451,531,411 baada ya Ruwasa kutekeleza mradi huo kwa kuwatumia mafundi wa kawaida.
Aidha, alitaja mradi mwingine unaotekelezwa ni katika kijiji cha Masuguru ambao unatarajia kuhudumia wananchi wapatao 3,264 na gharama za mradi huo ni Sh.402,000,000.
Kwa upande wake msimamizi wa mradi huo Gloria Nziku alisema,mradi wa maji katika kijiji cha Msuguru unatekelezwa chini ya program ya malipo kwa matokeo na ulianza kutekelezwa mwezi Agosti mwaka 2021 na unatarajia kukamilika tarehe 30 mwezi huu.Nziku,ameishukuru wizara ya maji kutoa fedha na serikali ya kijiji na wananchi,kwa ushirikiano mkubwa waliotoa wakati wa utekelezaji wa mradi huo ambao hadi sasa umefikia asilimia 85.Alisema,mradi utakapokamilika jumuiya ya watumia maji Masuguru ndiyo watakuwa wasimamizi wakuu na waendeshaji wa mradi huo.
Amewataka viongozi wa jumuiya na wananchi kuhakikisha wanalinda miundombinu ya mradi ili uendelea kufanya kazi kama ilivyokusudiwa na serikali.
Mkazi wa kijiji hicho Dolfina Chowo alisema,wanachangamoto kubwa yam aji safi na salama ambapo wanatumia maji ya visima vya kupampu na wakati mwingine maji ya visima na mito iliyopo kando ya kijiji hicho.
Alisema, sasa wana matumaini makubwa ya kuondokana na kero hiyo baada ya serikali kupitia wakala wa maji safi na usafi wa mazingira(Ruwasa)kuanza kutekeleza mradi wa maji ya bomba ambao umeanza kuleta matumaini makubwa kwao.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.