Mkuu wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma Mhe. Peres Magiri, amekabidhi gari jipya kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), Wilaya ya Nyasa gari lililotolewa na Wizara ya Maji kwa lengo la kutatua kero ya usafiri kwa mamlaka hiyo.
Hafla ya makabidhiano ya gari hilo imefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Nyasa na kuhudhuriwa na watumishi pamoja na wananchi wa Wilaya ya Nyasa.
Ameishukuru Serikali kwa kuipa Wilaya ya Nyasa gari ambalo linakwenda kutoa huduma ya usafiri wa uhakika na kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.
Malengo ya Serikali, ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2025, wananchi wote waishio Vijijini katika Mkoa wa Ruvuma, wanafikiwa na kupata huduma ya maji safi na salama kwa asilimia 85 na ifikapo 2030 wanapata huduma maji kwa asilimia 100.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.