Katika eneo la Migelegele, wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma, kung’ara kwa Sekondari ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ni ushahidi wa wazi wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuwekeza kwa vitendo kwenye elimu bora kwa wote. Shule hii mpya, yenye majengo ya kisasa, maabara za kisayansi, maktaba na mabweni ya kuvutia, imekuwa mkombozi mkubwa kwa wanafunzi wa kike wa maeneo ya pembezoni waliokuwa wakitembea umbali mrefu kufuata elimu ya sekondari.
Leo, ndoto zao za wasichana za kusoma katika mazingira bora zinatimia kwa sababu ya uwekezaji huu wa kimkakati ulioasisiwa kwa jina la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.