Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefungua rasmi shule ya mfano ya wasichana katika Mkoa wa Ruvuma, wilayani Namtumbo. Shule hiyo imegharimu shilingi bilioni 4.35 kukamilika.
MAJENGO NA UWEZO WA SHULE
Makamu Mkuu wa shule, Bw. Bernad Komba, amesema ujenzi wa shule umejumuisha jengo la utawala moja (1), madarasa ishirini na mawili (22), bwalo moja la chakula (1), mabweni tisa (9) kwa wanafunzi, maabara nne (4), maktaba, na chumba cha TEHAMA. Shule hiyo ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,200, lakini kwa sasa ina wanafunzi 548 kutoka kidato cha kwanza, cha tano, na cha sita.
Kufikia Januari mwaka huu, shule hiyo inatarajia kupokea wanafunzi 128 wa kidato cha kwanza, na hivyo kuongeza idadi ya wanafunzi kufikia 700.
FAIDA KWA WANAFUNZI WA KIKE
Mwanafunzi Groli Gama amepongeza jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea shule yenye mazingira rafiki na wezeshi, yanayowapa nafasi wanafunzi wa kike, wakiwemo wenye ulemavu, kujifunza bila changamoto yoyote.
Shule hii imekuwa mfano wa kuigwa kwa kuboresha mazingira ya elimu kwa wasichana, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuinua sekta ya elimu nchini.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.