Afisa Elimu Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mwl Patrick Haule ameishukuru serikali kwa kutoa mabilioni ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya tano za sekondari kupitia program ya Uboreshaji Elimu ya Sekondari (SEQUIP).
Akizungumza ofisini kwake mjini Tunduru Haule amesema katika Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa SEQUIP serikali ya Awamu ya Sita ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 1.5 za ujenzi wa sekondari tatu mpya katika kata za Nakayaya,Majimaji na Lukumbule.
Amesema shule zote zimekamilika na zimechukua wanafunzi wa kidato cha kwanza wapatao 500 katika shule zote tatu mwaka huu
Amesema shule hizo zimesaidia kupunguza utoro wa wanafunzi ambao walikuwa wanasafiri umbali mrefu wa kilometa kati ya 15 hadi 20 hali iliyosababisha wanafunzi wengi kuacha shule.
“Takwimu zinaonesha kuwa kati ya wanafunzi 6000 waliokuwa wanaanza kidato cha kwanza Halmashauri ya Tunduru ni wanafunzi 1800 pekee ndiyo walikuwa wanamaliza kidato cha nne “,alisema Haule.
Hata hivyo Haule ameishukuru serikali kwa kutoa fedha nyingine kupitia program ya SEQUIP kujenga sekondari mbili mpya katika kata za Tuwemacho na Tinginya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru ambapo kila shule itajengwa kwa shilingi milioni 560.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.