Serikali imekamilisha miradi mbalimbali ya kuboresha huduma za afya katika hospitali ya Wilaya ya Tunduru, mkoani Ruvuma.
Miradi hiyo ni pamoja na ukarabati wa Hospitali ya Wilaya kwa gharama ya shilingi milioni 900. Hospitali hiyo kongwe iliyojengwa mwaka 1930 baada ya kuboreshwa miundombinu inatoa huduma kwa ubora wa hali ya juu.
Pia, jengo la wagonjwa wa dharura lililogharimu zaidi ya shilingi milioni 300 limekamilika na vifaa tiba vya kisasa vimewekwa ambapo Jengo hilo litaimarisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa wa dharura.
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Tunduru Dr.Bernad Mwamanda amesema serikali imetoa gari la wagonjwa ambalo litasaidia kusafirisha wagonjwa kwa ufanisi, tofauti na awali ambapo hospitali ilitegemea kuazima magari kutoka vituo vingine.
Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt. maboresho haya yamepunguza changamoto za utoaji huduma.
“Tunaishukuru serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu yetu na kuhakikisha huduma bora zinapatikana kwa wakati,” alisema Dkt. Mwamanda.
Huduma bora za afya sasa zinapatikana katika Hospitali ya Wilaya ya Tunduru, jambo ambalo linatajwa kuinua hali ya afya ya wananchi wa eneo hilo.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.