SERIKALI imewataka Wananchi mkoani Ruvuma kurasimisha viwanja vyao kwani itapelekea kupanda kwa thamani katika maeneo yao pia kuepusha migogoro isiyo ya lazima wao kwa wao
Wito huo umetolewa na Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Ruvuma Idefonce Ndemela, Wakati akizungumza katika hafla iliyofanyika hivi karibuni ya utoaji hati 57 kwa wananchi wa kata ya Ruhuwiko Songea mkoani Ruvuma.
Alisema ni muhimu wananchi kuelewa maana ya urasimishaji kwani itasaidia kuepusha migogoro pia amesema kupitia zoezi hilo wao kama ofisi ya ardhi mkoa wameamua kumpunguzia mwanchi mdaa mwingi wakufuatilia hati na badala yake wao wanamfuata mwananchi alipo
“Niwashukuru wote ambao mmefikia hatua ya kupewa hati leo kwa kutambua umuhimu wa kurasimisha Ardhi pia tungependa zoezi hili litokee na meeneo mengine kwa uwingi wenu inaleta maana kuwa wezetu wengine bado awajarasimisha maeneo yao hivyo tuwahamasishane kwani hati zinapatikana hapa hapa mkoani,” Alisema Ndemela
Hata hivyo Diwani wa kata ya Ruwiko Wilbert Mahundi, amewasisitiza wananchi wake watambue kuwa zoezi hilo linamanufaa kwao hii ni baada ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali za mipaka hivyo urasimishaji ardhi ni dhamana kwao pia uondoa migogoro
“Tulianza zoezi hili kwa muda mrefu kwa kuamua kurasimisha maeneo yetu ili tuweze kuyamiliki kisheria kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, ardhi ni mali ya serikali sisi wananchi tunayaendeleza kwa utaratibu kwa kufuata sharia,”alisema Mahundi.
Naye Frank Mhagama mkazi wa kata ya Ruhuwiko ameishukuru ofisi ya Ardhi Mkoa wa Ruvuma, kwa kuweza kufanya zoezi hilo kwa muda mfupi na kuwapatia hati hizo kwa wakati kwani zinawapa uhuru wa kuwazesha katika mambo mbalimbali ikiwemo kupata mikopo
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.