• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI kuanza ujenzi wa kituo cha Afya Matiri Mbinga

Imewekwa kuanzia tarehe: August 25th, 2022

WAKAZI  13,000 wa kata ya Matiri Halmashauri ya wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma,wanatarajiwa kuondokana na kero ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya matibabu baada ya Halmashauri ya wilaya kuanza ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha  Matiri.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa kituo hicho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbinga Juma Haji kwa mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas,Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo George Mhina alisema,lengo la kujenga kituo hicho ni kuboresha huduma za afya ya jamii na kuleta ukombozi kwa wananchi.

Alisema,kazi za ujenzi ikiwamo kusafisha eneo la ujenzi kwa kushirikiana na wananchi wa kata hiyo zilianza mwezi Februari mwaka huu na zilitarajiwa kukamilika tarehe 30 ,lakini kutokana na changamoto ya hali ya hewa wanatarajia kukamilisha mradi huo mwezi Septemba.

Kwa mujibu wa Mhina,kazi ya ujenzi wa mradi huo zinaendelea vizuri ambapo hadi sasa hatua iliyofikiwa inaridhisha  kwani jengo la wagonjwa wa nje(OPD) na maabara yako katika hatua ya kupaka rangi.

Alitaja, kazi nyingine zinazoendelea ni jengo la upasuaji,jengo la mama na mtoto  na jengo la kufulia nguo ambayo yapo katika hatua ya kupiga lipu na mategemeo katika awamu ya pili  jengo la mama na mtoto na jengo la kufulia nguo yatakamilika katika kipindi cha miezi mitatu.

Mhina ambaye ni Katibu wa afya wa Halmashauri ya wilaya alieleza kuwa,mradi hadi utakapokamilika utagharimu jumla ya Sh.milioni 500 zilizotolewa na Halmashauri ya wilaya na mchango wa wananchi ni Sh.milioni 11  na hadi sasa fedha zilizotumika ni Sh.milioni  379.

Mhina alisema, malengo ya Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi wa kata hiyo ni kukamilisha ujenzi wa mradi  huo  kwa wakati kwa kuzingatia uwajibikaji na kuweka maslahi ya mradi mbele.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kazi nzuri ya kusimamia makusanyo ya ndani na kutekeleza vyema miradi mbalimbali  inayolenga kuchochea maendeleo kwa wananchi.

Alisema,Halmashauri zikikusanya vizuri mapato yake zitakuwa na uwezo wa kujiendesha na kutekeleza mipango iliyojiwekea badala ya kutegemea ruzuku kutoka Serikali kuu au kwa wahisani.

Kanali Laban amezitaka Halmashauri nyingine katika mkoa huo kuiga mfano wa Halmashauri ya Mbinga  katika ukusanyaji madhubuti wa mapato ya ndani na kutekeleza miradi ya  mbalimbali ya maendeleo pasipo kusubiri msaada kutoka kwa watu wengine.

Kanali Laban,amewapongeza wananchi wa kata  ya Matiri kwa kuchangia fedha zaidi ya Sh.milioni 11 katika ujenzi wa mradi huo na kuwataka kushirikiana na Halmashauri yao ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.Katika hatua nyingine,mkuu wa mkoa amewaomba wananchi wa wilaya ya Mbinga kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 23 mwezi huu kwa ajili ya kushiriki zoezi la sense ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Alisema,zoezi la sensa ya watu na makazi ni muhimu sana kwa maendeleo na uchumi wa nchi yetu kwani inatoa nafasi kwa serikali kutambua idadi ya watu wake na kamwe zoezi hilo halihusiani na itikadi za  vyama vya siasa.

“ndugu zangu wa Mbinga kama tutafanya kosa mwaka la kutojitokeza kwa wingi kuhesabiwa basi tutafanya kosa kubwa ambalo litasababisha kukosa taarifa na takwimu sahihi za watu wake”alisema.

Mbunge wa Jimbo la Mbinga vijijini Benaya Kapinga ameipongeza Halmashauri kwa kutenga fedha kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha huduma za afya,ambapo kwa mwaka 2022 inajenga vituo vitatu vya afya vya Matiri,Muungano na Mkumbi.

MWISHO

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • KIONGOZI mwenge wa Uhuru aonya rushwa kwenye uchaguzi

    May 10, 2025
  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.