Akiongea kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mchomoro wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma Mwezeshaji Edigna Muhule ambaye pia ni afisa mifugo wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alitoa kauli ya marufuku kwa wanufaika wa kaya maskini kutumia vibarua katika ajira ya muda inayotolewa na Tasaf .
Muhule aliwafafanulia wananchi lengo la serikali la kuweka ajira ya muda kwa wanufaika wa fedha za kaya maskini ni kuwaongezea kipato hivyo kitendo cha wanufaika hao kuwaajiri vibarua kuwafanyia kazi ni kinyume na malengo ya serikali.
Hata hivyo Muhule alidai serikali kupitia utekelezaji wa miradi mipya inakuja na utaratibu wa kuwatambua wanufaika wa kaya maskini ambao hawawezi kufanya kazi za ajira za muda kulingana na umri wao hao wataendelea kupokea fedha ya kumtambua kuwa kaya maskini pamoja wategemezi wake kama awali lakini wanufaika wale wenye uwezo wa kufanya kazi watafanya kazi za muda hawatahusika na kile kiasi walichokuwa wanapokea awali kwa kuwa ajira ya muda itawapatia fedha za kutosha kupitia kazi wanazofanya huku wategemezi wakibaki na malipo yao kama wanasoma shule .
Mratibu wa Tasaf wilaya ya Namtumbo Hyasint Mbiro alisema utambulishaji wa miradi mipya ya Tasaf wilayani Namtumbo ina enda sambamba na utoaji elimu ya namna miradi hiyo itakavyotekelezwa kwa kupitia wanufaika wa fedha za kaya maskini Tasaf ili waweze kujiongezea kipato.
Mbiro aliwataka wanufaika wa kaya maskini kujitokeza kufanya kazi ya ajira ya muda ili kujiongezea kipato kwa kuwa ajira hiyo ndiyo inawawezesha kupata fedha nyingi ukilinganisha na ruzuku wanazolipwa.
Pamoja na hayo Mbiro aliwataka wanufaika wa kaya maskini kuhakikisha anahudhuria kazini siku zote za kazi na kuwahimiza kuandika mahudhurio mara baada ya muda wa kazi kumalizika na kutojiorodhesha katika daftari la mahudhurio ukiwa kazini kutawakosesha fedha alisema Mbiro.
Saidi Ntali mnufaika wa fedha za kaya maskini kijiji cha Mchomoro alionesha wasiwasi wake kwa mwezeshaji huyo kuwa bila kufanya kazi fedha za kila mwezi walizokuwa wakipata zitaenda wapi alisema Ntali.
Adamu Zuberi mnufaika wa kaya maskini kijiji cha Mchomoro aliwashukuru wawezeshaji na wataalamu kutoka ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri wilaya ya Namtumbo kwa kuwafafanulia utaratibu na mwongozo wa malipo ya Tasaf na kuondoa sintofahamu ambayo ilianza kujitokeza katika malipo ya Tasaf kutokana na kukosa uelewa wa namna malipo hayo nyanavyofanyika badala ya kuwalaamu viongozi wao.
Zuberi aliwaomba wataalamu kutochoka kutoa elimu hiyo kwa wanufaika hao kwa kuwa wakati mwingine watu hulalamika kutokana na kukosa uelewa utaratibu na kuhisi kuibiwa .
Katika kijiji cha mchomoro Tasaf imetambulisha mradi mpya wa kujenga kivuko badala ya mradi wa visima sita katika kijiji hicho kuelekea katika hatua za mwisho za ukamilishaji.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.