Mkoa wa Ruvuma leo umeanza kutoa mafunzo ya siku mbili ya Utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 kwa Timu za uendeshaji wa Huduma za afya Mkoa (RHMT) na Halmashauri(CHMT) pamoja na maafisa habari wa Halmashauri.
Mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Jairy Khanga amesema, lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wataalamu wa afya kwenda kutoa huduma za chanjo kwa wananchi kwa kutoa elimu ya kuwaelimisha wananchi umuhimu wa chanjo ya UVIKO 19, kwa kuvifikia vituo vyote vya kutolea Huduma na Kata na Vijiji.
Dkt Khanga ameongeza kuwa mafunzo ya siku mbili kwa wataalamu wa afya, watawezeshwa njia na mbinu za kuelimisha jamii pamoja na kupambana na changamoto zitakazopatikana kutoka kwa wananchi aweze kutoa elimu ya kuwaelimisha wananchi na waweze kuchanjwa.
‘’Wananchi hawana taarifa sahihi kuhusu chanjo ndio maana mwamko wa wananchi katika swala la kuchanja ni dogo hivyo tunatakiwa kuimarisha dhana ya mawasiliano na kuwafanya wananchi wengi waweze kupata tarifa sahihi na kubadilisha fikra potofu walizonazo na wakubali kuchanja alisema” Dkt Khanga
Hata hivyo aliwataka watoa huduma za chanjo katika mkoa wa Ruvuma kushiriki mafunzo ya siku mbili ya kujengewa uwezo katika utoaji chanjo katika Halmashauri za wilaya zote za mkoa wa Ruvuma kwa lengo la kuwafanya wananchi wahamasike katika zoezi la kuchanja kwa kuwa moja ya changamoto iliyopo katika jamii ni elimu juu ya chanjo hiyo haijatolewa katika jamii.
Aidha amempongeza Afisa Afya na mazingira wa Halmashauri ya wilaya ya Tunduru bwana Arnold Herman na mratibu wa elimu ya afya kwa jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Ally Yassin Ndambile kwa kuhamasisha jamii kuhusu kupata chanjo hiyo.
William Reuben kiongozi wa timu ya kitaifa ya chanjo katika mkoa wa Ruvuma amewataka washiriki wa mafunzo kuleta matokeo katika kazi watakazotakiwa kwenda kuzifanya ili kutekeleza lengo la serikali la kuhakikisha wananchi wake wanapata chanjo .
Mada zinazofundishwa katika mafunzo hayo ni mada 8 ambapo kwa siku ya kwanza mada ya sayansi ya jamii,mawasiliano juu ya chanjo ,mabadiliko ya tabia , utaratibu na usimamizi shirikishi kwa jamii na mada zingine 4 zitafundishwa siku ya pili.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.