• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Majibu ya haraka |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • RSFMIS |
Ruvuma Region

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Elimu
      • Miundombinu
      • Maji
      • Afya
      • Menejimenti ya Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
      • Tehama
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Songea
    • Wilaya ya Mbinga
    • Wilaya ya Nyasa
    • Wilaya ya Tunduru
    • Wilaya ya Nantumbo
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya ya Madaba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mji
    • Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
    • Halmashauri ya Wilaya ya Songea
    • Halmashauri ya Manispaa ya Songea
    • Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru
  • Fursa za Uwekezaji
    • Mifugo
    • Kilimo
    • Vivutio vya Utalii
    • Madini
    • Nyaraka za uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
  • Machapisho
    • Miongozo na Nyaraka za uwekezaji
    • Taratibu
    • Taarifa
    • jarida
    • fomu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • habari
    • Matukio

SERIKALI yakabidhi vifaa tiba mtandao hospitali ya Rufaa Ruvuma

Imewekwa kuanzia tarehe: May 23rd, 2022


 Sasa wagonjwa kupata huduma  bobezi za  kibingwa ndani ya Mkoa wa Ruvuma

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imekabidhi vifaa vya tiba mtandao katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma hali ambayo itawawezesha wananchi kupata huduma bobezi za kibingwa  ndani ya Mkoa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo katika Hospitali ya  Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma,Mwakilishi wa Wizara ya Afya ambaye pia ni Mratibu wa  Tiba Mtandao,Dr. Ligile Vumilia amesema huduma hiyo ni muhimu hasa kwa wananchi wanaoishi pembezeni kama Mkoa wa Ruvuma.

Amesema wananchi wote ambao watakuwa wanahitaji huduma za afya za kibingwa na bobezi sasa watazipata katika hospitali ya Rufaa ya Ruvuma badala ya kusafiri umbali mrefu ambapo serikali imeichagua hospitali hiyo kuwa ni miongoni mwa hospitali  tano za mwanzo  kabisa nchini kupatiwa huduma hiyo.

Dr.Vumilia amesema kuletwa kwa vifaa hivyo katika hospitali ya  Rufaa Mkoa wa Ruvuma ni kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipofanya uzinduzi wa X-Ray katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma mwaka 2019,aliagiza kuanzisha huduma ya tiba mtandao katika hospitali hiyo.

“Serikali kupitia Wizara ya Afya imeichagua Hospitali  za Rufaa za Ruvuma,Bombo Tanga, Mkoa wa Katavi na hospitali mbili za Wilaya za Nzega na Chato kuwa hospitali za mwanzo kufungiwa huduma ya tiba mtandao’’,alisisitiza Dr.Vumilia.

Amesema  Mfuko wa Mawasiliano kwa wote umetoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya kununua vifaa tiba mtandao  kwa ajili ya hospitali tano nchini na kwamba vifaa vya tiba mtandao vinapelekwa katika hospitali hizo na vitaunganishwa kwajili ya kuanza kazi ya kutoa huduma za kibingwa kwa wagonjwa.

Hata hivyo amesema Taasisi ya Teknolojia nchini inatarajia kufunga vifaa vya tiba mtandao baada ya makabidhiano hayo ambapo katika hospitali ya Rufaa ya Ruvuma chumba maalum kimeshaandaliwa kwa ajili ya kufungwa vifaa hivyo.

Kwa mujibu wa Mratibu huyo,huduma hiyo inatarajiwa kutolewa katika hospitali za Rufaa 21 nchini na kwamba huduma ya tiba mtandao katika hospitali hizo itaunganishwa na hospitali za Kanda za Bugando Mwanza,Kanda ya Benjamin Mkapa Dodoma na Kanda ya Mbeya.

“Tutakuwa na hospitali nne za kitaifa ambazo zitakuwa na huduma bobezi za kibingwa ambazo ni hospitali ya Taifa Muhimbili,hospitali ya mishipa na mifupa ya fahamu ya MOI,hospitali ya saratani ya Ocean Road na  Taasisi ya Jakaya Kikwete ambayo ni maalum kwa magonjwa ya moyo’’,alisisitiza Dr.Vumilia.

Amesema huduma ya tiba mtandao katika hospitali ya Rufaa ya Ruvuma itamwezesha mgonjwa yeyote kupata huduma bobezi za kibingwa bila kusafiri umbali mrefu kama hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa  ya Mkoa wa Ruvuma Dr.Magafu Majura amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa msaada wa vifaa vya tiba mtandao ambao utawawezesha wananchi kufanyiwa vipimo mkoani Ruvuma na vipimo hivyo kutumwa kwa njia ya mtandao hivyo mgonjwa kufahamu ugonjwa wake akiwa Ruvuma hivyo kupunguza gharama za usafiri na malazi kwa mgonjwa.

“Kwa kutumia vifaa vya tiba mtandao tutakuwa sawa na waliopo Dar es salaam,wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na nchi jirani za Msumbiji na Malawi sasa watapata huduma za kibingwa wakiwa Songea’’,alisisitiza Dr.Majura.

Naye Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Afya Catherine Sungura amesema serikali pia imetoa shilingi milioni 630 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma na kwamba katika nchi nzima serikali inajenga majengo ya wagonjwa wa dharura katika hospitali nane za rufaa.

Sungura amesema pia serikali imetoa shilingi milioni 150 kwa ajili ya ukarabati wa jengo la wagonjwa mahututi (ICU) katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma ambapo miradi yote hiyo imetekelezwa kwa asilimia 100.

Imeandikwa na Albano Midelo

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Mkoa wa Ruvuma

Machi 23,2022

Matangazo

  • JARIDA la RS Ruvuma toleo la Aprili 2025 April 30, 2025
  • VIGEZO vya kupata leseni ya biashara September 30, 2025
  • FURSA za uwekezaji mkoani Ruvuma June 30, 2025
  • ORODHA ya nyumba za kulala wageni mkoani Ruvuma December 31, 2025
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • MWENGE wa Uhuru waikubali miradi yote Madaba

    May 09, 2025
  • RC Ruvuma ALIVYOSHIRIKI Makabidhiano mradi wa ujenzi wa Chuo cha Uhasibu Songea

    May 08, 2025
  • SERIKALI yatenga bilioni 18.5 kujenga chuo kikuu Ruvuma

    May 08, 2025
  • MWENGE wa Uhuru kukagua,kuzindua miradi 76 Ruvuma

    May 08, 2025
  • Tazama zote

Video

HAKIKISHA unafika kanisa la Peramiho-Rais Samia
Video Zaidi

Viungio vya Haraka

  • Songea Municipal Council
  • Mbinga District Council
  • Tunduru District Council
  • Madaba District Council
  • Nyasa District Council
  • Namtumbo Dictrict Council
  • Mbinga Town Council
  • Songea District Council

Tovuti Muhimu

  • Utumishi Portal
  • Government Portal
  • Tamisemi
  • Tanzania Revenue Authority

Waliotembelea Kijiografia

world map hits counter

Waliotembelea

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Regional Commissioner Office

    Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 S.L.P 74,SONGEA, RUVUMA.

    Simu: 0252602256

    Simu ya Mkononi: KERO PIGA 0800110174

    Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Majibu ya haraka
    • Ramani ya Mahala
    • Huduma

Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.