MKUU wa Wilaya ya Songea Mkoa wa Ruvuma Pololeti Mgema amezindua zoezi la ugawaji wa Hati miliki kwa wananchi zaidi ya 30.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Kata ya Ruhuwiko Manispaa ya Songea amesema ziko sababu za kupewa hati miliki ya ardhi.
Mgema amesema hati miliki ya ardhi inasaidia kukuza uchumi kwa kujipatia mikopo benk pamoja na kutatua migogoro katika maeneneo yaliyo pimwa.
“Huko nyuma aliyekuwa Waziri wa ardhi Profesa Anna tibaijuka aliwahi kusema natamani kila kipande cha ardhi katika nchi yetu kipimwe na kumilikishwa.
Amesema hati miliki inatolewa kwa mujibu wa Sheria namba 4 ya ardhi ya mwaka 1999 na kuundwa sheria nyingine namba 5 ya vijiji ya mwaka 1999 na kupeana hati miliki ya kimila ikiwa mtu hatakiwi kumili zaidi ya hekari 50 ndani ya ardhi ya kijiji.
Kamishna msaidizi wa ardhi wa Mkoa wa Ruvuma Idefonce Ndemela katika zoezi hilo amesema zoezi hilo limezinduliwa na wananchi waondoe dhana ya upatikanaji wa hati ni shida .
“ Hati inapatikana kwa masaa machache ndiomana tumekuja na hati ambazo mwananchi atasaini hapa na msajili atasajili hapa na kamishna atasaini na watajipatia hati zao leo”.
Ndemela amesema zoezi hili walianzisha tangia mwaka 2021 katika halmashauli na matokeo yake yamekuwa makubwa na kufikia asilimia 80,na amesema zoezi hili halitaishia hapa litakuwa endelevu pale wananchi watakapokuwa wamelipia ankra zao watafikiwa.
Afisa ardhi Mteule Manispaa ya Songea Theresphory Komba amesema jumla ya viwanja zaidi ya 2400 vimepimwa na michoro ya mipango miji 10 imeandaliwa katika maeneo ya Ruhuwiko Kanisani na wananchi zaidi ya 30 watapewa hati zao.
Imeandaliwa na Aneth Ndonde na Jackson Mbano
Kutoka kitengo cha Mawasiliano Serikalini Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Juni 23,2022.
Regional Commissioner Office
Anuwani: 1 TUNDURU ROAD, 57180 SONGEA, RUVUMA.
Simu: 0252602256
Simu ya Mkononi: 0252602256
Barua Pepe: ras.ruvuma@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Ruvuma . All rights reserved.